Katibu Mkuu Ujumbe wa Video Siku ya Wakimbizi Duniani 20 June 2018

Ungalifanya nini iwapo ungelazimishwa kuondoka nyumbani kwako?

Hii leo, zaidi ya watu milioni 68 duniani kote ni wakimbizi au wakimbizi wa ndani kutokana na mizozo au mateso.

Hii ni sawa na idadi ya watu kwenye nchi ya 20 kwa ukubwa zaidi duniani.

Mwaka jana, katika kila sekunde mbili mtu mmoja alikimbia makazi.

Hasa katika nchi maskini zaidi.

Katika siku ya Wakimbizi Duniani, lazima tufikirie tufanye nini zaidi ili kusaidia.

 

Jibu linaanza na umoja na mshikamano.

Nina wasiwasi mkubwa kushuhudia mazingira zaidi ambamo wakimbizi hawapati ulinzi wanaohitaji na ambao ni haki yao.

Tunahitaji kuanzisha tena maadili ya mfumo wa kimataifa wa ulinzi wa wakimbizi.

Katika dunia ya leo, hakuna jamii au nchi ambayo inatoa hifadhi salama kwa wakimbizi wanaokimbia vita au mateso inapaswa kuachwa pekee yake au bila msaada.

Tusimame pamoja au tushindwe. 

Mwaka huu, Mkataba wa kimataifa kuhusu wakimbizi yatawasilishwa mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Unatoa mwelekeo wa mbele na kutambua michango ya wakimbizi katika jamii zinazowahifadhi.

Alimradi kuna vita na mateso, wakimbizi wataendelea kuwepo.  

Katika siku ya Wakimbizi Dunia, nakuomba uwakumbuke.

Simulizi zao ni za mnepo, uvumilivu na ujasiri.

Zetu zinapaswa kuwa za mshikamano, upendo na vitendo.

Asanteni.