Remarks by UN Resident Coordinator at Inauguration of beach wall on Barack Obama Drive in Dar es Salaam on World Environment Day

 

 

REMARKS OF UN RESIDENT COORDINATOR and UNDP RESIDENT REPRESENTATIVE, MR. ALVARO RODRIGUEZ AT THE INAUGURATION OF THE OCEAN ROAD WALL

DURING THE WORLD ENVIRONMENT DAY

5 JUNE 2018

 

Your Excellency, Samia Suluhu Hassan, Vice President of the United Republic of Tanzania,

Hon. January Makamba, Minister of State, Vice President’s Office for Union and Environment

Hon. Kangi Lugola, Deputy Minister, Vice President’s Office for Union and Environment

Hon. Paul Makonda, Regional Commissioner, DSM Region

Colleagues, representatives from UN agencies, development partners and members of the press,

Excellencies, honoured guests, ladies and gentlemen.

Habari za Asubuhi na Asalam Aleikhum!

Kwa niaba ya Wafadhili wa Maendeleo, na Familia ya Umoja wa Mataifa, tunatoa pongezi kubwa, kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa  jitihada zinazoendelea, katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, na changamoto za kimazingira. Katika kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani, Tanzania imeendelea kuonyesha  dhamira ya kweli ya kushiriki na  kufikia malengo ya dunia na mpango wa Taifa wa  miaka mitano. Mpango unaotambua umuhimu wa utunzaji wa mazingira, na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Kwa hili ninasema hongereni sana!

 

Ni heshima kubwa kwa Umoja wa Mataifa kuwa mshirika wa miradi  mabalimbali ya mazingira na mabadiliko ya Tabia Nchi; ambapo leo hii tunashuhudia, moja ya matokeo ya miradi hii, kwa uzinduzi wa ukuta huu. Shukrani za kipekee kwa UNEP, UNOPS wakishirikiana na Serikali ya Tanzania, ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, kuhakikisha ukuta huu unajengwa kwa muda muafaka na wenye kulinda mazingira ya kando na ndani ya bahari.

Umoja wa Mataifa unatambua juhudi za serikali katika kuleta maendeleo ya haraka na yenye tija kwa wananchi wake. Tunaahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania na wadau wa Maendeleo kuhakikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu yanafikiwa. Malengo haya ni pamoja na kutunza mazingira yetu.

Mheshimiwa Rais,

Naomba nichukue fursa hii tena kukupongeza kwa uongozi wako, wenye kujali maslahi ya watanzania wengi, kwa upana wake, huku ukiipeleka nchi katika kufanikisha malengo ya Maendeleo Endelevu ifikapo mwaka elfu mbili na thelathini.

Umoja wa Mataifa, utaendelea kufanya kazi na wadau wake wote, kuhakikisha maendeleo endelevu kwa nchi ya Tanzania.

Tuko pamoja kulijenga taifa letu.

Pamoja tunaweza!

Asanteni Sana!