UJUMBE WA SIKU YA KIMATAIFA YA WALINDA AMANI

KATIBU MKUU

--

UJUMBE WA SIKU YA KIMATAIFA YA WALINDA AMANI

                                                             29 MEI 2018

 

Tarehe 29 Mei mwaka 1948 , Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliidhinisha operesheni ya kwanza ya ulinzi wa amani ya Umoja wa Mataifa– Mpango wa usimamizi wa mapatano Mashariki ya Kati.

 

Katika maadhimisho haya ya miaka 70, tunatoa shukrani zetu kwa zaidi ya wanaume na wanawake milioni moja ambao wamehudumu wakibeba bendera ya Umoja wa Mataifa na kuokoa maisha yasiyohesabika ya watu.

 

Tunawaenzi zaidi ya walinda amani 3,700 waliolipa gharama kwa kupoteza maisha yao.

 

Na tunazienzi operesheni 14 zinazofanya kazi usiku na mchana kuwalinda watu na kuendeleza mchakato wa amani.

 

Mwaka huu naitumia siku ya kimataifa ya walinda amani duniani nikiwa nchini Mali ili kuonyesha mshikamano wangu na wenzetu ambao wanakabiliwa na idadi kubwa ya majeruhi na hali tete.

Tunapotambua umuhimu wa huduma na kujitolea kote duniani, pia ninasimama kidete kuchukua hatua kwa ajili ya walinda amani- hatua za kufanya operesheni zetu kuwa salama na za ufanisi zaidi katika mazingira ya leo yenye changamoto.

 

Pia tumejizatiti kuimarisha jukumu muhimu ambalo vikosi vyetu vinastahili kulitekeleza katika kuchagiza haki za binadamu na kukabiliana na unyanyasaji na ukatili wa kingono.

 

Ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa ni thibitisho la uwekezaji wa amani, usalama na ustawi duniani.

 

Kwa pamoja, hebu tuahidi kufanya kila tuwezalo ili kufanikisha mpango huo.

 

Asanteni.