Remarks by UN Resident Coordinator at opening ceremony of TAGCO Capacity Building Programme

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Hotuba ya Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa, Tanzania 

Ndg. Alvaro Rodriguez

Mkutano wa Wanahabari wa Serikali

ARUSHA, Jumatatu, 12 Machi 2018, Ukumbi wa AICC

  • Mh. Dr. Harrison Mwakyembe, Waziri, Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo
  • Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na 
  • Wajumbe wa  TAGCO
  • Wanahabari

 

MABIBI NA MABWANA,

Habari za Asubuhi na Asalamu Aleikhum. Nichukue fursa hii ya kipekee kuwashukuru sana waandaaji wa mkutano huu kwa kutupa nafasi muhimu sana kukutana nanyi siku ya leo. Pia nichukue fursa hii kuwapongeza  wana mawasilaino kutoka serikalini ambao ni wanachama wa TAGCO. Umoja wa Mataifa unatoa pongezi sana kwa mkutano huu na tunaamini malengo yatakayoafikiwa yataleta tija kubwa sana katika maendeleo ya nchi yetu ya Tanzania! Hongereni sana.

Kama wadau wa maendeleo na kiongozi ninayethamini mawasiliano; ningependa kuzungumzia mambo makuu matatu:

  1. Kwanza: Dunia inabadilika kwa kasi ya haraka sana na kwa mara ya kwanza katika historia ya Dunia, tunaishi katika dunia iliyounganika kupitia teknolojia. Muunganiko huu ni muhimu sana, lakini umeleta hali ya habari za uongo “Fake news” wakati mwingine.  Hivyo basi serikali ina umuhimu mkubwa wa kufundisha na kuhabarisha jamii kuhusu matumizi sahihi ya teknolojia zinazotuunganisha. Lakini, serikali hiyo hiyo, inahitaji kusikiliza jamii, kwani ni sauti za wananchi na hii itafanikisha kupata maendeleo ya haraka kwa Tanzania.
  2. Umoja wa Mataifa unaiona Tanzania ya leo na kesho yenye mafanikio mengi sana. Demokrasia, kufikia uchumi wa kati, Elimu bure, kupiga vita rushwa ni kati ya vitu vinavyoipa Tanzania sifa ya nchi iliyo tayari kuleta maendeleo ya nchi kwa ajili ya wananchi. Yote haya tunayajua kupitia kwenye mikono yenu kama wana mawasiliano. Niwape pongezi kwani mnaunganisha serikali na wadau mbalimbali kupitia mawasiliano. Lakini sisi kama wadau wa maendeleo, tungependa kusikia zaidi maendeleo ya jamii hasa  za vijijini yanavyobadilika kutokana na sera nzuri za Serikali ya Tanzania. Haya ndio mawasiliano kwa ajili ya maendeleo “communication for development.” Pia tungependa kusikia kupitia mawasiliano yenu, ni jinsi gani mpango wa miaka mitano umefanikiwa na changamoto zake.  Hivyo basi ni muhimu sana kuielewa na kuiwasilisha  Tanzania kupitia mpango wa Taifa wa miaka mitano – 5YDP na MKUZA III.
  3. Kama Umoja wa Mataifa, tungependa kuwa washirika wa Serikali katika mawasiliano ya maendeleo nchini, kwani sisi pia ni watumishi wa umma. Kazi zetu ni kusaidia katika kutekeleza malengo ya dunia – Sustainable Development Goals kama ilivyopewa kipaumbele katika mpango wa Taifa wa Maendeleo   - 5YDP na MKUZA III.  Ni kwa maana hiyo basi tunaamini kuwa Umoja wa Mataifa kupitia wana mawasiliano wake wakishirikiana na Serikali kupitia wana mawasiliano wake, tutaweza kuijua Tanzania ya viwanda, Tanzania ya maendeleo, Tanzania tunaiyotaka, Tanzania ya leo na ya kesho. Hivyo basi tunategemea kufikia makubaliano ya ushirikiano wetu  kesho ambapo tutasaini makubaliano kati ya Mawasaliano Umoja wa Mataifa na TAGCO. Yote hii ni kuhakikikisha tunaonyesha matokeo chanya yanayofanywa na Serikali ambapo sisi kama Umoja wa Mataifa tupo kusaidia kufanikisha malengo hayo.

 

Nimalizie kwa kusema: TUFANYE YA WAKATI, WAKATI TUNA WAKATI; UTAKUJA WAKATI TUKITAKA KUFANYA YA WAKATI, WAKATI HATUNA WAKATI. WAKATI NI HUU! TAGCO HOYEE!

 

Asanteni Sana NA Kila la kheri!