Press Releases

Jamii mkoani Kigoma zanufaika kutokana na Umoja wa Mataifa

TAARIFA YA HABARI KWA VYOMBO VYA HABARI

                                        

 

Imezuiwa hadi saa 6 kamili mchana, Aprili 11, 2018

 

Jamii mkoani Kigoma zanufaika kutokana na Umoja wa Mataifa

Vijana mkoani Kigoma wanufaika na msaada wa UN

Kigoma, 11 Aprili, 2018 –Umoja wa Mataifa ulizindua Mpango wa Pamoja wa Kigoma (KJP) mwaka jana kwa lengo la kuunganisha mwitikio wa sasa wa Umoja wa Mataifa kwa tatizo la wakimbizi na wahamiaji huku mkazo mkubwa ukiwa katika kuziendeleza jamii za wenyeji. Mpango huo ulizinduliwa kwa ushirika na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kundi la Washirika wa Maendeleo, vyombo vya habari, Mashirika ya Kiraia, jamii za wenyeji wa wakimbizi na wahamiaji za mkoani Kigoma. Mpango huo wa KJP unahusisha mashirika 16 ya Umoja wa Mataifa yakishirikiana katika maeneo makuu sita. Wakiongozwa na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez, leo Kundi la Mawasiliano la Umoja wa Mataifa (UNCG), maofisa 15 kutoka mashirika ya UN nchini Tanzania, mamlaka za serikali za mitaa na vyombo vya habari waliwatembelea vijana na wanawake walionufiaka na programu ya pamoja ya UN ya awali katika Mji wa Kigoma.

KJP vilevile inaendeleza jitihada zilizofanywa hapo kabla na UN kama vile mradi wa pamoja wa UN uliofadhiliwa na ILO, UNIDO, UNWOMEN na FAO kwa vijana. Programu ya pamoja iliendeshwa kwa kushirikiana na AZISE ya maalia, Nyakitonto Youth For Development Tanzania, Manispaa ya Kigoma. Zaidi ya vijana 110 walipata mafunzo ya uendelezaji huduma za biashara. Vijana waliopewa mafunzo hivi sasa wanaendesha biashara katika maeneo ya kilimo, kilimo cha mbogamboga na matunda na utengenezaji sabuni.

Ziara ya uwandani ilifanyika katika eneo la uzalishaji la mmoja wa vijana waliopewa mafunzo katika Kituo cha Vijana cha Nyakitonto. Vijana waliopewa mafunzo kama sehemu ya programu walionyesha baadhi ya shughuli zao za ujasiriamali kama vile utengenezaji sabuni. Akizungumza wakati wa ziara ya uwandani, Mratibu Mkazi wa UN, Bw. Alvaro Rodriguez, alisema kwamba “Matokeo ya programu ya pamoja iliyotangulia iliyofanywa na mashirika ya UN kwa kushirikiana na Nyakitonto yanaonyesha tunaweza kupata matokeo chanya tunaposhirikiana kwa karibu na jamii za wenyeji katika mkoa.” Aliongeza kwamba, “Tunavyoendelea kutekeleza Mpango wa Pamoja wa Kigoma, tunalenga kuendeleza matokeo haya na hatimaye kupanua KJP katika mkoa mzima. Kwa kushirikiana na Norway, KOICA na Sweden, UN iko ili kuisaidia serikali kuhakikisha kwamba hatua zinazochukuliwa za kiutu hazizuii maendeleo.”

Bw. Rodriguez vilevile alivipongeza vyombo vya habari vinavyofanya kazi mkoani Kigoma kwa utayari wao wa kuendelea kushikiana na vyombo vya habari ili kufanya utetezi wa masuala ya kimaoendeleo yanayoshughulikwa na UN kupitia KJP na jitihada nyingine mkoani humo.

Matini/Maelezo ya nyongeza kwa Wahariri:

Utekelezaji wa KJP ulianza mwezi Julai, 2017. Programu inajumuisha jumla ya mashirika 16 ya UN yanayofanya kazi katika maeneo makuu sita ambayo ni nishati endelevu na mazingira; uwezeshaji kiuchumi vijana na wanawake; kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto; elimu; kilimo; na WASH (maji, usafi wa mazingira na usafi binafsi). Programme hiyo inatekelezwa katika wilaya tatu ambazo zina zaidi ya wakimbizi 300,000. Wilaya hizo ni Kasulu, Kibondo na Kakonko.

 

Kama ilivyoonyeshwa na vijana walionufaika na Mpango huu wa Pamoja wa UN huko Kigoma Mjini, UN nchini Tanzania imekuwa ikizisaidia jamii za wenyeji mkoani Kigoma hata kabla ya kuanza kwa KJP. Vilevile, akiwa mkoani Kigoma, Mratibu Mkazi wa UN alikutana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Generali Mstaafu Emmanuel Maganga, kujadiliana vipaumbele vya maendeleo katika mkoa huo.

 

Kwa taarifa zaidi kuhusu Programu ya Pamoja ya Kigoma, tafadhali tembelea:

tz.one.un.org/kigoma-joint-programme/overview

 

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na:

 

Bi. Hoyce Temu                                                                                             

Mtaalamu wa Mawasiliano                                                                

Ofisi ya Mratibu Mkazi

Umoja wa Mataifa Tanzania

Baruapepe: +255 682 262 627

Wavuti:    http://tz.one.org

Instagram: @unitednations_tz

Facebook: United Nations Tanzania

Twita:    @UnitedNationsTZ, @Alvaro_UNTZ

 

-30-