Ujumbe kutoka kwa Bi Irina Bokova, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Siku ya Urithi wa Afrika Duniani

Mei 5, 2017

 

Siku ya Urithi wa Afrika Duniani ni fursa ya kusherehekea utajiri wa utamaduni na asili ya bara, asili ya ubinadamu. Pia ni wakati kufaa kutoa onyo kwa ajili ya ulinzi wa urithi wetu. Leo maeneo ishirini na tatu (23) ya Afrika yapo kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia katika Hatari – Mji Mkongwe wa Ghadamès, Hifadhi ya Kahuzi-Biega, na Hifadhi ya Asili ya Mlima Nimba Mkali – ziko hatarini kutoweka kama hatutachukua hatua za haraka ya kuzilinda. Kila moja ana jukumu hilo.

Hatua ya kulinda urithi barani Afrika sasa, ina uunda maisha yetu ya baadaye. Kusaidia jamii - na hasa vijana - ili kukuza na kuendeleza rasilimali nyingi za kitamaduni na asili ina maana ya kuandaa mipango ya muda mrefu, zinazo zinagatia maendeleo itakayoletwa na umoja an ushikamano wa jamii. Maeneo ya Afrika zinalindwa zaidi na jamii zinazoishi kando yao kila siku na kupata utambulisho wao kupitia huu urithi na kuendesha maisha yao kutokana na mapato wanazopata kupitia kwao. Usimamizi yao ni endelevu zaidi ukiongozwa na vijana ambao wanatambua umuhimu yao. Azimio ya Ngorongoro, iliyopitishwa mwaka 2016, inahamasisha kuendeleza jukumu la jamii, hasa ya vijana na wanawake, katika usimamizi wa maeneo ya urithi wa dunia. Ujumbe huu inaendelea kuwa muhimu leo.

Ulinzi imara inahitaji elimu, habari sahihi na utafiti. Hii ndiyo sababu UNESCO katika kutekeleza wajibu ya kulinda urithi wa Afrika inasimamia katika kazi yake ya kuelimisha na kusambaza uelewa wa umuhimu wa urithi kuptia elimu ya maadili ya kuvumiliana, kuheshimiana na uelewa wa tamaduni. Katika Afrika, UNESCO inafanya kazi ya kuimarisha usimamizi ya maeneo katika programu ya chuo kikuu na mafunzo.

Leo, ninawaomba wadau wote wa Afrika, Nchi zote, vyama vya kiraia na za jamii kuchukua jukumu kwa ajili ya ulinzi wa mali ya Bara la Afrika zisizolinganishwa na bara nyingine kwa utajiri. Ningependa kuwashukuru kwa dhati, wale wote wanapambana kila siku, wakati mwingine hata kuhatarisha maisha yao, ili kulinda na kushiriki urithi huu wa kipekee wa binadamu wote. Hii ina ashiria nyayo zetu za zamani kuwakilisha msingi imara wa maadili, vigezo na kujiamini kwa maisha ya baadaye. Afrika ni tajiri kwa haya, na Maendeleo chanya yenye tija kwa Afrika inategemea kuendeleza urithi wa dunia la Afrika.