Ujumbe wa Mkurugenzi Mtendaji wa UN Women Phumzile Mlambo-Ngcuka wa Siku ya Wanawake duniani, Machi 8, 2017

 

Wanawake katika mabadiliko ya dunia ya kazi: Ulimwengu 50-50 kufikia mwaka 2030

Ujumbe wa Mkurugenzi Mtendaji wa UN Women Phumzile Mlambo-Ngcuka wa Siku ya Wanawake duniani, Machi 8, 2017

 

Kote duniani, wanawake na wasichana hutumia mda wao mwingi kwa kazi za nyumbani- kwa kukadilia zaidi ya mara mbili ya masaa ambayo hutumika na wanamme na vijana. Wanasaidia kutunza ndugu zao wadogo, wazee, kushughulikia magonjwa kwenye familia na kusimamia nyumba. Kwa mara nyingi huu mgawanyo wa kazi usio sawa ni kwa gharama ya masomo ya wanawake na wasichana,kwa kazi ya kulipwa, michezo au ushiriki katika uongozi wa kiraia au jamii. Hii huchangia kwa kanuni za faida na hasara, ambapo wanawake na wanamme hupata nafasi katika uchumi, kwa yale ambayo wana ujuzi wa kufanya na mahali ambapo wanafanya kazi.

 

Huu ndio ulimwengu usiobadilika wa kazi isiyozawadiwa, tukio la kawaida la kimataifa la matumaini yaliyopotea, ambapo wasichana na mama zao huendeleza familia kwa kazi ya bure, kwa maisha ambayo asili yake ni tofauti na yale ya wanamme katika familia.

Tunataka kujenga ulimwengu tofauti wa kazi kwa wanawake. Wanapokua, wasichana lazima wapewe fursa ya kujishirikisha kwa aina tofauti za kazi, na kuhimizwa kufanya maamuzi yanayopita kiwango cha huduma za jadi na maamuzi ya mwelekezo kwa kazi za sekta, sanaa, utumishi wa umma, kilimo cha kisasa na sayansi.

Ni lazima tuanze kufanya mabadiliko kutoka nyumbani na kwa siku za mapema shuleni, ili kusiwe na pahali popote kwa mazingira ya mtoto ambapo watajifunza kwamba wasichana lazima wawe chini, wawe na machache na wawe na ndoto  kidogo kuliko wavulana.

Hii italeta mabadiliko katika uzazi, mitaala, mazingira ya elimu na njia za kila siku za televisheni, matangazo na burudani;  itasaidia kuchukua hatua thabiti za kukinga wasichana wadogo kutokana na tamaduni mbaya kama ndoa za utotoni, na kutokana na aina nyingine za unyanyasaji.

Wanawake na wasichana ni lazima wawe tayari kujishirikisha kwa mfumo wa kisasa wa mapinduzi. Kwa sasa asilimia 18 ya shahada za kwanza za sayansi compyuta zimeshikililiwa na wanawake. Ni lazima tuone ubadilifu mkubwa kote duniani kwa wasichana  kuchukua  masomo ya STEM,kama wanawake watashindana kwa ufanisi za ajira mpya za kulipa zaidi.Hivi sasa asilimia 25 tu  katika mfumo wa kisasa wa viwanda ni wanawake.

 

Kufikia usawa katika sehemu za kazi itahitaji upanuzi wa kazi na fursa za kazi na ajira za heshima, kushirikisha juhudi za serikali za kukuza ushiriki wa wanawake katika maisha ya kiuchumi, msaada wa pamoja wa mashirika muhimu kama vyama vya wafanyakazi, na sauti za wanawake wenyewe katika kutunga ufumbuzi wa kuondokana na vikwazo vya sasa kwa ushiriki wa wanawake, kama ilivyochunguzwa na Jopo la Ngazi ya juu ya Uwezeshaji wa Wanawake Kiuchumi la Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.Vigingi ni vikubwa: kuendeleza usawa kwa wanawake kunaweza kuongeza pato la kimataifa kwa dola za Marekani trillioni 12 ifikapo mwaka 2025.
 
Pia inahitaji malengo makinifu katika kuondoa ubaguzi wanawake wanakabiliwa nao kutoka pande mbalimbali sababu ya jinsia zao: mwelekeo wa kijinsia, ulemavu, umri mkubwa, na ubaguzi wa rangi. Pengo la malipo hufuata baaada ya haya: pengo la mshahara wa wastani ni asilimia 23 lakini hili huongezeka hadi  asilimia 40 kwa wanawake wafrika wanoishi marekani. Katika Umoja wa Ulaya, wanawake wazee wana asilimia 37 zaidi ya uwezekano wa kuishi katika umaskini kuliko wanaume wazee.

 

Katika majukumu ambayo tayari wanawake wamewakilishwa zaidi lakini wanalipwa malipo ya chini, na pia kwenye kinga kidogo ya kijamii, ni lazima tufanye hayo mashirika kuwalipa wanawake vyema. Kwa mfano, uchumi wa utunzi mwema unaowajibika na mahitaji ya wanawake na kutoa ajira ya faida kwao; hali na masharti sawa kwa kazi ya waanawake inayolipiwa na isiyolipiwa; na ushirikiano na wanawake wawekezaji, ikiwemo upatikanaji wa fedha na masoko. Wanawake katika sekta isiyo rasmi lazima pia mchango wao uweze kukubaliwa na kulindwa. Huu ni mwito wa kuwezesha sera za uchumi ambazo zinachangia ukuaji wa pamoja na maendeleo makubwa kwa watu milioni 770 wanaoishi katika umaskini uliokithiri.

Kuzungumzia ukosefu wa haki utasababisha suluhisho na mabadiliko kutoka kwa waajiri walio katika sekta ya umma na ile ya kibinafsi. Motisha itahitajika ili kuajiri na kurejesha wafanyikazi wa kike; kama kupanua mafao ya uzazi kwa wanawake ambayo pia yanatasababisha urejeo katika kazi, kupitisha Kanuni za Uwezeshaji wa Wanawake, na uwakilishi wa moja kwa moja katika ngazi za kufanya maamuzi.

Kuandamana na haya, mabadiliko muhimu katika utoaji wa faida kwa baba wageni unahitajika, pamoja na mabadiliko ya kitamaduni ambayo yatafanya upewaji ya siku za mapumziko ya uzazi kuwa chaguo la faida, na hivyo kuchagia hali halisi ya faida za pamoja katika familia.

Katika utata huu, kuna mabadiliko madogo na makubwa yanahitajika kufanywa: kwa wanamme kutoa malezi, kwa wanawake kujishirikishana kwa waichana kuwa na uhuru wa kukua sawa na wavulana. Mabadiliko lazima yafanyike katika pande zote ikiwa tutakuwa na nia ya kuongeza idadi ya watu ambao wanaweza kujishirikisha katika kazi ya heshima, kuweka bwawa ili liwe la umoja, na kugundua faida ambazo zitapatikana kwa wote kutokana na dunia sawa ilivyotajwa katika agenda ya mwaka 2030 ya Maendeleo Endelevu.