Ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres

Ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres

 

Kutokomeza chuki na ubaguzi dhidi ya waislamu

 

New York, 17 Januari 2017

 

Nawashukuru nyote kwa kukutana kukabili changamoto ya chuki na ubaguzi dhidi ya waislamu. 

 

Vitendo vya uhalifu utokanao na chuki dhdi ya waislamu na aina nyingine za ukosefu wa stahmala vinaongezeka.

 

Suala hilo pia linahusu chuki dhidi ya wageni, ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wayahudi.

 

Halikadhalika, watu wengi ni wahanga wa ukosefu wa stahmala na hofu kuwa haviwezi kuonekana kwenye takwimu,  vinashusha utu wa mtu na ubinadamu wetu.

 

Mara nyingi, ukosefu wa usalama, jamii zenye shida na zenye muonekano tofauti ndio zinakuwa visingizio vya haraka. 

 

Lazima tukatae jitihada za kejeli za kugawanya jamii na kuona  jirani kama watu tofauti. 

 

Ubaguzi unatuteketeza sote. Unazuia watu na jamii kufikia uwezo wao waliojaliwa.

 

Hebu na tuimarishe uwezo wetu kwa kutumia maadili ya kujumuishana, stahmala na kuelewana ambayo ndio kitovu cha imani zote kubwa na katiba ya Umoja wa Mataifa.

 

Kama kurani tukufu inavyosema: mataifa na makabila yaliundwa ili kufahamiana. 

 

Watu popote walipo wanahitaji kuhisi kuwa utambulisho wao wa kitamaduni unathaminiwa– na wakati huo huo wajione wanakubalika katika jamii nzima. 

 

Kadri jamii zinavyokuwa na mjumuiko wa tamaduni na dini tofauti tofauti, tunahitaji uwekezaji wa kisiasa, kitamaduni na kiuchumi katika umoja, ili utofauti wetu uonekane kuwa ni rasilimali na si tishio.

 

Umoja wa Mataifa unazindua jitihada za kuendeleza heshima, usalama na utu kwa wote.  Tunaita Kampeni ya pamoja. 

 

Pamoja, hebu na tusimame kidete dhidi ubaguzi na haki za binadamu.

 

Pamoja, hebu tujenga madaraja.

 

Pamoja, hebu tubadili hofu iwe matumaini.  

 

Kwa ndugu zetu waislamu – na kwa binadamu wote. Asanteni.