Press Releases

UNDP yajenga vyoo vya Sh510m kusaidia usafi Kilimanjaro

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

Imezuiwa mpaka Halamisi Februari 16,2017. Mchana - Saa za Afrika Mashariki

 

UNDP yajenga vyoo vya sh 510,000,000 kusaidia usafi Kilimanjaro

 

“Usafi wa shule ni muhimu kwa mazingira bora ya utoaji elimu”

 

Februari 2017,Moshi Kilimanjaro - Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania ,  Alvaro Rodriguez, akishirikiana na Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy wamezindua vyoo kumi vilivyojengwa katika shule za Msingi kumi wilayani Moshi.

Ujenzi huo ulifanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya uwapo wa Umoja wa Mataifa.

Wakati wa maadhimisho hayo pia wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa walifanya shughuli mbalimbali mkoani Kilimanjaro za kusaidia maendeleo ikiwamo hifadhi ya mazingira na usafi.

Katika kuhakikisha kwamba shule zinakuwa na vyoo, UNDP Tanzania  ilisaidia  mkoa wa Kilimanjaro  Sh. 510,000,000 kujenga vyoo vya kisasa katika shule za msingi 10 ili kusaidia kuwezesha usafi kwa wanafunzi na walimu wao. Hadi kufikia leo jumla ya matundu 178 yamejengwa katika shule 10 ambapo matundu 104 ni kwa ajili ya wasichana na 74 kwa ajili ya wavulana.

Akizungumza katika uzinduzi huo mwakilishi mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez,alipongeza mradi huo na ushirikiano uliokuwapo kati ya serikali, wao na shule ikiwa ni hatua moja ya maendeleo endelevu kwa kuboresha mazingira ya usafi kwa wanafunzi wa kike na wa kiume katika masomo yao na hivyo kuimarisha safari ya kuelekea malengo ya dunia ya 2030.

Alisema kutokuwepo kwa mazingira bora ya usafi ni changamoto kubwa kwa wanafunzi na hali hiyo inawaaathiri sana wanafunzi wa kike.

Alisema kutokana na kujengwa kwa vyoo hivyo wanafunzi, walimu na walezi sasa watakuwa na kazi pekee ya kuhakikisha kwamba wanatoa elimu bora. Aidha watoto wa kike watakuwa na changamoto chache zaidi za mahudhurio shuleni na wakati huo huo masuala ya usafi yatakuwa yameboreka na hivyo kuwa na wanafunzi na familia zenye siha njema.

Naye Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy amepongeza kwa msaada huo na kuutaka Umoja wa Mataifa kuendelea kutoa msaada kwa shule zenye mahitaji makubwa kuhakikisha kwamba malengo ya dunia yanayohusiana na usafi, mazingira na maji safi yanafikiwa ifikapo mwaka 2030.

Alisisistiza kuwa misaada ya aina hii yenye malengo maalumu inasaidia utekelezaji wa lengo la la nne kuhusu elimu na lengo la sita la kuwa na maji safi na usafi na hivyo kusaidia kufikia lengo  kwa kutengeneza mazingira bora ya mafunzo kwa wote.

Balozi Mushy pia aliongeza: “Kama ilivyo ada kwamba hisani huanzia nyumbani , basi suala la usafi huanza kwako na kwangu.

Naye Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Sadick Meck Sadick pamoja na kuishukuru UNDP kwa kazi nzuri waliyoifanya pia alizitaka jumuiya za maeneo yaliyojengewa vyoo kumiliki  msaada huo kwa kuhakikisha wanaitunza na hivyo kusaidia kufikia malengo ya  dunia 2030.

Alisema kwamba binadamu ana eneo moja tu analoweza kuishi hivyo ni wajibu wake kulitunza. Alisema kwa sasa mazingira yanaharibiwa kwa kasi kutokana na kukosekana kwa utashi wa ulinzi wa mazingira. Ametaka tabia hiyo kubadilika na kila Mtanzania kuwa mlinzi wa mazingira kwa lengo la kutumia vyema fursa zilizopo kwa maendeleo.

Shule za msingi ambazo zilinufaika na mradi huo ni Mseroe, Fukeni, Majengo, Mrieny, Riata, Mue, Kiboroloni, Majengo, Azimio na Mandela.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa upo mkoani Kilimanjaro kwa siku tatu na umetembelea dawati la Jinsia Kituo cha polisi Moshi na kwenye chuo cha Polisi Moshi na katika miteremko ya mlima Kilimanjaro ambapo wakati wa maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa  miche 2,000 ya miti ilipandwa.

Pia ujumbe huo ulizuru Chuo Kikuu cha MUCCOBS , kilichopo Moshi ambako walienda kuhamasisha malengo ya dunia 2030 ,maendeleo endelevu.

 

Angalizo kwa wahariri:

Kwa miaka 50, Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) limekuwa mstari wa mbele katika kusukuma maendeleo, ujenzi wa taasisi , kuongeza ujasiri, kusaidia nchi kutekeleza mageuzi na kusaidia kuratibu misaada na imechangia kuwapo na mafanikio makubwa ya maendeleo katika nchi nyingi duniani.

Hapa nchini Tanzania, UNDP imekuwa kwa muda mrefu ikishiriki katika juhudi za maendeleo ya taifa kwa kusaidia katika maeneo muhimu kama demokrasi na utawala bora, mazingira  na mabadiliko ya tabia nchi, kupambana na umaskini wa kiuchumi, uratibu wa misaada na sasa inasaidia serikali ya Tanzania kuhuisha malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) na mipango ya ndani na ndani ya sera na dira za maendeleo.

 

Kwa habari zaidi juu ya Wiki ya Umoja wa Mataifa tafadhali wasiliana na:

 

Hoyce Temu

Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa

0682262627

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.